Header Ads

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KU DESIGN LOGO


Kubuni alama(logo) yaweza kuonekana ni kazi ngumu sana lakini usihofu endapo utapitia na kuzingatia sharia ma taratibu kadhaa ,basi utaunda logo/alama ambayo itadumu maishani na kuwa bora zaidi.Logo au alama yaweza kuwa ya mtu binafsi kampuni au hata taasisi na vikundi mbali mbali kama wewe ni graphics design mchanga au unaechipukia zingatia yafuatayo wakati unapobuni logo


1:MTAMBUE MTEJA WAKO
Kama unatengeneza logo kwa ajili ya mteja ambaye atakulipa ni muhimu sana kumtambua mteja wako kwa undani.Je ni kampuni au taasisi inayojihusisha na nini.Je ni langi gani mteja wako anazipenda ziwakilishe kampuni yake.Je wapinzani wake wanajihusisha na nini,kama ni taasisi inajihusisha na nini au nkama ni mtu binafsi yeye ni nani Msanii,Mwalimu, Photographer .Ukisha fahamu nenda hatua inayofuata


2:JADILI/CHANGANUA KWANZA MAWAZO YAKO
Jadili au changanua kwanza unachokiwaza kuhusu mteja wako na logo unayotaka kumuandalia
Chuku Penseli na Karatasi nyeupe na anza kuchora chora ideas tofauti tofauti.Kwani sikushauri ukae katika computer ufungue illustrator na uanze kufikilia .Kitakachotokea hakitakuwa kizuri .




3:ZINGATIA URAHISI
Hakuna mtu anayependa kuwa na logo ngumu kueleweka au yenye rangi zenye kukwaza
Kuapuka haya basi wakati unjadili wewe na akili yako basic hora angalau logo ambayo ni rahisi (simple and unique) Ikiwezekana tumia hata alama ilimradi iendane na profile ya mteja wako.

3:WASILISHA MAWAZO YAKO SASA KATIKA COMPUTER
Hapa namaanisha ideas zote ambazo ulizichora chora katika hatua ya pili jaribu kuzi design kwa kutumia program ambayo wewe unahisi unaiweza Ila nashauri sana tumia Adobe Illustartor , CorelDRAW kama huna atleast Adobe Photoshop.Chukua michoro yote na ichore katika hio programu.

4:WASILISHA MAPENDEKEZO YAKO
Baada ya kazi nzito ya kuzichora Idea zako tengeneza Document ( proposal document) ambapo utaziweka ideas za logo ambazo unahisi ni bora Zaidi ,zaweza zikawa tatu au nne angalau kisha muoneshe mteja wako na msikilize ipi ameipenda


5:KUBALI KUKOSOLEWA
Endapo mteja akakukosoa kubali na muelezee kwa hoja za kujenga naamini itakufanya ufikilie zaidi na ubuni kilicho bora .Pia Jaribu Kutoa sababu za kujenga na kujalibu kuangalia Je LOGO uliotengeneza itafaa kusimama na kuendana na Mwenendo wa soko la sasa duniani ?


6:VECTORIZE LOGO YAKO
Ku vectorize namaanisha kuifanya logo iwe katika muundo/format ya Vector ambayo vector unaweza ukaitanua ukubwa au udogo pasipo kupungua Ubora scalable

7:IBORESHE
Ifanyie maboresho mpaka utakapoona sasa iko tayari

8:MWISHO

Hatua ya mwisho kabisa ni kuiweka logo katika size tofauti  na kuiwasilisha kwa mteja wako .

1 comment:

Powered by Blogger.